LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ndege za ATCL kusafirisha shehena za samaki kwenda nje ya nchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (pichani), leo Januari 15, 2019 amefanya ziara ya kutembelea viwanda vinavyochakata minofu pamoja na mabondo ya samaki Jijini Mwanza na kubaini uwepo wa shehena za kutosha kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Mhandisi Kamwele amesema hatua inayofuata ni kuliimarisha zaidi shirika la ndege nchini ATCL kwa ajili ya kusafirisha shehena ya minofu ya samaki kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza hadi nje ya nchi tofauti na hivi sasa ambapo baadhi ya wenye viwanda wamekuwa wakitumia viwanja vya ndege vya Nairobi Kenya ama Entebe nchini Uganda.

Pia Mhandisi Kamwelwe amekagua ujenzi wa eneo la mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwanza ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 89 ikiwa ni pamoja na miundombinu yake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki Jijini Mwanza cha Nileperch Limited, Rupesh Mohan, baada ya kiutembelea kiwanda hicho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha Nileperch Limited Jijini Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe  (kushoto), akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha kuchakata samaki cha Natures Fish Limite. Kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho ambapo amemshukuru Waziri Kamwelwe kwa kuonyesha utayari wa ndege za ATCL kusafirisha monofu ya samaki kwenda nje ya nje na kusema itawapunguzia gharama za usafirishaji.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe na msafara wake  akikagua kiwanda cha mabondo ya samaki cha Rhong Zeng Tanzania Ltd.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.