LIVE STREAM ADS

Header Ads

“Ole wake atakayefanya biashara nje ya masoko ya madini”- Biteko

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Wizara ya Madini, Doto Biteko akiwasilisha salamu za Wizara hiyo kwenye ziara ya Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan katika Wilaya ya Iramba mkoani Singida, hii leo Februari 20, 2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) ameungana na viongozi mbalimbali kushiriki katika ziara ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (hayuko pichani) mkoani Singida ambapo katika Wilaya ya Iramba, Mama Samia amekagua kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti cha Yaza kinachomilikiwa na mwekezaji mzawa kilichopo eneo la Ndago, ujenzi wa Kituo cha Afya Kinampanda pamoja na ukarabati wa Chuo cha Ualimu Kinampanda na baadae kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.
Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema Serikali kupitia Wizara hiyo inatarajia kuanzisha masoko ya madini hapa nchini, hivyo wafanyabiashara wote watapaswa kuuzia madini yao kwenye masoko hayo.

Biteko ametoa kauli hiyo hii leo kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Wilaya ya Iramba mkoani Singida ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi aliyoianza Februari 16, 2019 mkoani humo.

No comments:

Powered by Blogger.