LIVE STREAM ADS

Header Ads

Makamu wa Rais aanza ziara ya kikazi mkoani Tabora

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Simbo uliopo Wilaya ya Igunga mkoani Tabora ulipofanyika mkutano wa hadhara ikiwa ni sehemu ya ziara yake wilayani humo iliyoanza leo Februari 21, 2019. Pamoja naye ni viongozi mbalimbali akiwemo mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa Tabora, Agrey Mwanri.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan alisimama katika Kijiji cha Bulyang'ombe, Kata ya Nanga wilayani Igunga kusalimiana na wananchi waliojitokeza barabarani kumlaki.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan alikagua ujenzi wa tanki la maji katika eneo la Mwamaganga ambalo litapokea maji katika mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria unaogharimu shilingi bilioni 600.
Sehemu ya majengo yaliyojengwa katika Kituo cha Afya Sembo wilayani Igunga ambapo Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amefika kukagua upanuzi wa Kituo hicho.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akipanda mche wa mti katika Kituo cha Afya Simbo baada ya kukagua upanuzi wa Kituo hicho kilichopewa shilingi Milioni 400 kwa shughuli hiyo kupitia mfumo wa "Force Account".
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akipanda mche wa mti katika Kituo cha Afya Simbo baada ya kukagua upanuzi wa Kituo hicho kilichopewa shilingi Milioni 400 kwa shughuli hiyo kupitia mfumo wa "Force Account".
Mkuu wa Mkoa Tabora, Agrey Mwanri akipanda mche wa mti katika Kituo cha Afya Simbo.
Baadhi ya ananchi katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora wakimsikiliza Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassa alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Simbo wilayani humo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.