LIVE STREAM ADS

Header Ads

NHC wazindua zoezi la uuzaji viwanja wilayani Chato

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Wananchi na wawekezaji mbalimbali wametakiwa kuchangamkia fursa ya uuzaji viwanja zaidi ya elfu moja vya makazi na biashara katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita ambavyo tayari vimepimwa katika Kata ya Muungano.

Akizungumza jana kwenye uzinduzi wa zoezi la uuzaji wa viwanja hivyo, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt. Maulid Banyasi alisema zoezi hilo linasimamiwa na NHC kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Chato.

Naye Mkuu wa Wilaya Chato, Mtemi Msafiri alishauri kuundwa Kamati Maalum ya uuzaji wa viwanja hivyo hatua itakayosaidia kuondoa malalamiko ikiwemo baadhi ya watu kupata viwanja vingi huku wengine wakikosa.
Na Joel Maduka, Geita
Tazam BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.