LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkataba wa ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Misungwi wasainiwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Halmashauri ya Wilaya Misungwi mkoani Mwanza imeingia mkataba na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wenye thamani ya shilingi bilioni 2.9 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Halmashauri hiyo utakaodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kisena Mabuba amesema ujenzi wa ofisi hizo zitakazojengwa katika Kata ya Igokelo utaondoa adha ya upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza ari kwa watumishi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa weledi zaidi tofauti na hivi sasa ambapo wanatumia ofisi zilizo katika jengo la Mkuu wa Wilaya Misungwi.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi, Antony Bahebe ameahidi ushirikiano wa kutosha ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu katika eneo la ujenzi ikiwemo maji na umeme ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Meneja wa TBA mkoani Mwanza, Khamis Kileo amesema mradi huo utakamilika kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa ili kufikia thamani ya fedha zilizotolewa na serikali kuu kwa Halmashauri hiyo ya Misungwi iliyoanzishwa mwaka 1995.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.