LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkutano wa Bunge la Afrika waanza nchini Afrika Kusini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE), Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi (pichani) akifungua mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Rais wa Bunge la Afrika, Roger Nkodo Dang akizungumza kwenye mkutano huo.
Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE),Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi (katikati), Rais wa Bunge la Afrika, Roger Nkodo Dang pamoja na washiriki wa mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika wakiimba wimbo wa Umoja wa Afrika.
Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa wakiimba wimbo wa Umoja wa Afrika.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele (kulia) na viongozi mbalimbali wa bunge hilo wakiwa kwenye mkutano huo.
Wabunge wa Bunge la Afrika wakiwa ukumbini.
Bunge linaendelea.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Aliyekuwa mjumbe wa uongozi wa Bunge la Afrika Dr. Bernadette Lahai kutoka Sierra Leone akitoa tamko na ujumbe wa mshikamano barani Afrika.
Wabunge wakiwa ukumbini.
Baadhi ya wabunge wapya wa bunge la Afrika kutoka Swaziland wakila kiapo.
Wabunge wapya wa bunge la Afrika wakila kiapo.
Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini.
Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini.
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika nchini Afrika Kusini.
Rais wa Shirikisho la Baraza la Taifa la Falme za Kiarabu (United Arab Emirates – UAE), Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi amefungua mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika ulioanza jana Mei 6, 2019 jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini kwa kukutanisha wabunge kutoka nchi 54 barani Afrika. 

Dr. Amal Abdullah Al Qubaisi alisema Bunge la Nchi za Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE) limekubaliana kushirikiana na Bunge la Afrika katika kumaliza changamoto zinazowakabili wananchi barani Afrika.

"Uhusiano wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Bara la Afrika umekuwa mkubwa, tumekuwa tukisaidia mambo kadha wa kadha barani Afrika, tunataka kuona usalama unazidi kuimarika Afrika, kwani bila usalama katika nchi zetu hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa" alisema Dr. Amal.

"Masuala ya vitendo vya kigaidi yana athari kubwa,tunatakiwa kwa pamoja kushirikiana kuyatafutia ufumbuzi ili wananchi wetu wawe salama lakini pia kuwa na suluhisho la kudumu juu ya wakimbizi wanaorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani,tunafurahi kuona wakimbizi wakirudi kwenye nchi zao kwa amani" aliongeza.

Kwa upande wake, Rais wa Bunge la Afrika, Roger Nkodo Dang alisema ili ushirikiano na umoja madhubuti unahitajika ili kufikia suluhu za kudumu juu ya masuala ya amani na usalama barani Afrika.

Ufunguzi wa mkutano wa pili wa kawaida wa Bunge la Afrika litakalofungwa Mei 17, 2019 ulikwenda sambamba na wabunge 26 wapya wa bunge la Afrika kutoka nchi mbalimbali Afrika kuapishwa.

Kauli mbiu ya Bunge la Afrika mwaka huu ni "2019 mwaka wa wakimbizi wanaorejea nyumbani na wakimbizi wa ndani, kuelekea kupata masuluhisho ya kudumu katika kulazimishwa kuhama makazi katika Afrika".

No comments:

Powered by Blogger.