LIVE STREAM ADS

Header Ads

Siri tatu muhimu kwa wenye uchu na mafanikio

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Mwl. Fabian Fanuel
Kila mtu duniani anatamani mafanikio ya aina mbalimbali. Mafanikio hayaji kirahisi ila yanakuja kwa utaratibu uliyoweka na kuandaliwa kwa umakini mkubwa. Pamoja na hayo inategemea malengo aliyonayo mtu pamoja na imani yake kwa Mungu.

Kimuziki kuna waimbaji wamefanikiwa sana, wengine kwa wastani huku wengine bado. Sasa ikiwa wewe ni mwanamuziki ili ufanikiwe, kuna sababu mbalimbali zinazosababisha hilo litokee ingawa inategemeana mtu kwa mtu.

1. Kutambua thamani ya ulichonacho (Knowing What you have Inside and how big and strong it is). Ukubwa wa kile ulichonacho ndani yako unatofautiana na mtu mwingine. Wewe ndiye unajua umebeba nini kwa uzito gani. Mafanikio yako yatakuja kutokana na uvumilivu jitihada na uthubuthu ulionao. Waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali walifanya bidii na kujifunza kwa waliofanikiwa, huku kila siku wakiweka nia na imani kuwa wanaweza, mfano "YES I CAN". Tambua una kitu kikubwa ndani yako na usikubali kushindwa kirahisi. Mungu yupo upande wako.

2. Kutambua muziki na mahitaji yake (Having music knowlegde and it's needs). Lazima ujue muziki ni nini na una mahitaji gani. Tambua muziki unahitaji nini na nini. Unatakiwa kujua aina tofauti za ala za muziki, kujua uwezo wa sauti yako na kujua sauti yako ikiimba aina gani ya muziki inakuwa inaoana. Epuka kufanya muziki kwa kufuata mkumbo au ushawishi wa watu. Penda kujifunza, fanya mazoezi na kuwa mtu wa sala na maombi mara kwa mara ili Mungu akupe kibali, neema, upenyo na upendelezo wa wazi.

3. Mungu akupe watu wa kusudi lako (Right people for God' purpose to you).
Lazima umwombe Mungu akupe watu sahihi kwa kusudi sahihi ulilonalo ndani yako. Waimbaji wengine wameshindwa kufanikiwa maana wamekutana na watu wasio wa kusudi lao. Wamewapoteza na kuwaharibia utaratibu wa kile walichonacho. Unatakiwa upate watu sahihi kwenye maombi, washauri wazuri na wewe mwenyewe kujua mipaka yako na watu wanaokuombea na kukushauri kihuduma. Waimbaji waliofanikiwa kuna watu nyuma yao wanaowasukuma  kwa mambo mengi.

No comments:

Powered by Blogger.