LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wafanyakazi wa “Power Banana” wafurahia Utalii katika Kisiwa cha Saanane

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wafanyakazi wa kampuni ya Mwanza Quality Wines ya jijini Mwanza inayozalisha mvinyo wa matunda wa Power Banana wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane jana Ijumaa Juni 28, 2019 ikiwa ni sehemu ya motisha kwa wafanyakazi hao kutoka kwa kampuni hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wafanyakazi hao wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Power Banana, Leopord Lema akipiga picha na mamba aliyekuwa akiota jua katika lango la kuingilia kwenye Kisiwa cha Saanane kilichopo ndani ya Ziwa Victoria jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa Power Banana wakiwasili kwenye Kisiwa cha Saanane kwa kutumia boti iendayo kasi.
Moja ya boti ziendazo kasi zinazotoa huduma ya utalii katika Kisiwa cha Saanane jijini Mwanza.
Mwongoza Watalii katika Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane, Lusubilo Steus (mbele katikati) akiwatembeza wafanyakazi wa Power Banana walipotembelea hifadhi hiyo.
Wafanyakazi wa kinywaji cha Power Banana wakiwa kwenye picha ya pamoja ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane jijini Mwanza.
Moja ya ndege aina ya Tausi wanaofugwa katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane.
Wafanyakazi wa Power Banana wakiendelea kufurahia utalii wa ndani ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane jijini Mwanza.
Hapa pia kuna Simba na wanaonekana mubashara kwa uzuri zaidi.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Power Banana wakiwa kwenye keji ya Simba.
Pundamilia wanaonekana kwa uzuri ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane jijini Mwanza.
Wanyama aina ya Nyumbu wakiwa kwenye hifadhi hiyo.
Swala wa aina mbalimbali pia wanapatikana ndani ya hifadhi.
Wanyama jamii ya nyani/ tumbiri pia wanapatikana ndani ya hifadhi.
Mwongoza Watalii katika Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane, Lusubilo Steus (kulia) akitoa mwongozo, ufafanuzi na maelezo mbalimbali kwa wafanyakazi wa kiwanda cha Power Banana walipotembelea hifadhi hiyo.
Burudani na michezo mbalimbali ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Power Banana wakiwa kwenye picha ya pamoja walipofika kwenye eneo lenye kimo cha juu (Jumping Point) ndani ya hifadhi ya Saanane.
Eneo zuri kwa ajili ya watalii kuruka juu na kupiga picha (Jumping Point).
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.