LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mashindano ya UMITASHUMTA 2019 yafana mkoani Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Katibu Tawala Mkoa Shinyanga, Albert Msovela (katikati) akizungumza wakati wa kufunga Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA 2019) katika uwanja wa CCM Kambarage jana Juni 11,2019. Kulia ni Kaimu Afisa Elimu Mkoa Shinyanga, Dedan Rutazika na kushoto ni Afisa Michezo Halmashauri ya Wilaya Shinyanga, Joseph Bihemo.
Katibu Tawala Mkoa Shinyanga, Albert Msovela akizitakia mchezo mwema timu zilizofuzu fainali ya mashindano ya UMITASHUMITA 2019 Mkoa Shinyanga ambazo ni Halmashauri ya Msalala (jezi rangi ya Machungwa) na Halmashauri ya Wilaya Kishapu (jezi za Bluu).
Kaimu Afisa Elimu Mkoa Shinyanga, Dedan Rutazika akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya UMITASHUMTA 2019.
Katibu Tawala Mkoa Shinyanga, Albert Msovela akisalimiana wachezaji wa timu ya Kishapu.
Katibu Tawala Mkoa Shinyanga, Albert Msovela akisalimiana wachezaji wa timu ya Msalala.
Mtanange kati ya Msalala na Kishapu ukiendelea ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika hakuna aliyefanikiwa kuona lango la mwenzake wakalazimika kwenda kwenye matuta na timu ya Msalala kuibuka na ushindi wa magoli 5 -4.
Mchezaji wa timu ya Kishapu akiipatia goli timu yake.
Walimu na wanafunzi wa Msalala wakishangilia baada ya kuichapa Kishapu magoli 5 -4.
Mchezo wa fainali kati ya timu ya wasichana ya Halmashauri ya Kishapu (wenye jezi nyeupe) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (jezi za bluu) ukiendelea.
Mchezo wa fainali kati ya timu ya wasichana ya Halmashauri ya Kishapu (wenye jezi nyeupe) na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (jezi za bluu) ukiendelea ambapo Manispaa ya Shinyanga waliibuka washindi kwa kuifunga Kishapu magoli 18 - 11.
Mchezo wa mpira wa netiboli kati ya timu ya wasichana Halmashauri ya Kahama Mji na Msalala ukiendelea. Kahama Mji walipata magoli 20 huku Msalala ikipata magoli 19.
Mchezo kati ya timu ya Halmashauri ya Kishapu (wenye jezi za bluu) na Halmashauri ya Shinyanga ukiendelea ambapo Halmashauri ya Shinyanga waliichapa Kishapu bao 1-0.
Shangwe zikiendelea uwanjani.
Vijana wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa uwanjani.
Meza kuu wakiwa wamesimama tayari kwa kugawa zawadi kwa washindi wa mashindano ya UMITASHUMTA 2019 mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa Shinyanga, Dedan Rutazika akikabidhi zawadi ya makombe kwa washindi katika michezo yote. Washindi wa jumla kuwa ni Halmashauri ya Wilaya Shinyanga na washindi mpira wa miguu kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, usafi Manispaa ya Shinyanga, Riadha Shinyanga, pete/ netiboli Manispaa ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde1 Blog
Katibu Tawala Mkoa Shinyanga, Albert Msovela amefunga Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA 2019) mkoani humo ambapo Shule kutoka Halmashauri sita za Wilaya zimeshiriki. 

Akifunga mashindano hayo jana Jumanne Juni 11,2019 katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, Msovela alisema hataki kuona wanafunzi kutoka Shinyanga wanashiriki mashindano ya UMITASHUMTA 2019 kitaifa mkoani Mtwara,bali anataka vijana hao wakarudi na makombe ya kutosha. 

"Nataka mkalete makombe badala tu ya kuwa washiriki wa mashindano ya UMITASHUMTA kitaifa,naamini kabisa vijana wetu wameandaliwa vya kutosha na tutachagua kikosi imara kitakachotuletea ushindi katika mkoa wetu" alisema Msovela. 

Aidha aliwataka wanafunzi watakaokwenda kushiriki mashindano hayo kitaifa kuwa na nidhamu ya kutosha na wakaoneshe vipaji vyao huku akiwakumbusha kuwa michezo ni ajira. 

Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Mkoa Shinyanga, Dedan Rutazika alisema ili kuleta ushindi wa kishindo, wataunda timu ya ushindi yenye vipaji maalum. 

Rutazika aliitaja miongoni mwa michezo iliyokuwepo wakati wa mashindano ya UMITASHUMTA 2019 yaliyofunguliwa mkoani Mei 27,2019 na Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainab Telack kuwa ni mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana, netiboli, riadha, riadha maalumu iliyohusisha watoto wasiosikia, Goalball (kwa wasioona), ngoma na kwaya. 

Aliongeza kuwa washindi katika michezo yote wamejipatia zawadi ya makombe huku akiwataja washindi wa jumla kuwa ni Halmashauri ya Wilaya Shinyanga na washindi mpira wa miguu kuwa ni Halmashauri ya Wilaya Msalala, usafi Manispaa ya Shinyanga, riadha Shinyanga, pete/ netiboli Manispaa ya Shinyanga.

Kauli mbiu ya mashindano ya UMITASHUMTA mwaka 2019 ni "Michezo na Sanaa kwa Elimu Bora na Ajira".

No comments:

Powered by Blogger.