LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanahabari wa mtandaoni wapigwa msasa kuhusu Habari za Uchunguzi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwezeshaji katika mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi, Charles Kayoka akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) yanayofanyika jijini Dodoma.
#BMGHabari
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Arusha, Claude Gwandu akifungua mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Charles Kayoka akisikiliza hoja kutoka kwa washiriki.
Mwezeshaji wa mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi, Charles Kayoka (kushoto) akisisitiza jambo kwa washiriki.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia jambo kwa njia ya mtandao kwenye afunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo.

Washikiri wakifuatilia mafunzo hayo.

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya mtandaoni wakifuatilia mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media/ Blogs/ Online TV) kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania, wamepatiwa mafunzo kuhusu namna ya kuandika habari za uchunguzi "Investigative Journalism" ili kuandika kwa weledi habari zinazohusu utetezi na ushawishi kwa kutumia takwimu (Data Driven Advocacy- DDA).

Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza leo Jumatano Julai 17, 2019 jijini Dodoma ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa utetezi na ushawishi wa Haki za binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).

Mradi huo unatekelezwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kupitia ya Klabu Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani chini ya taasisi za Freedom House pamoja na PACT.
Picha: Kadama Malunde & Albert Gsengo

No comments:

Powered by Blogger.