LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mongella azindua Kliniki Tembezi kusaidia upatikanaji wa huduma za afya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amezindua rasmi huduma ya Kliniki Tembezi (Mobile Clinic) yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za afya hususani kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI katika maeneo yenye changamoto ikiwemo visiwani.

Uzinduzi huo ulifanyika Jumamosi Aprili 25, 2020 jijini Mwanza ambapo huduma hiyo ya Kliniki Tembezi yenye nyenzo sawa na Kituo cha Afya itakuwa inapatikana kupitia gari maalum pamoja na boti. 

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa FIKIKA unaotekelezwa na shirika la ICAP linalosaidia mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI.
Na George Binagi-GB Pazzo-BMG
 Gari lililotengenezwa maalum kwa ajili ya kutoa huduma za afya (Kliniki Tembezi/ Mobile Clinic) mkoani Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma hiyo.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza akipima afya ndani ya Kliniki Tembezi.
Boti ililotengenezwa maalum kwa ajili ya kutoa huduma za afya (Kliniki Tembezi/ Mobile Clinic) mkoani Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari za Afya

No comments:

Powered by Blogger.