LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mvua zaleta madhara Sengerema “dereva asombwa na mafuriko”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani Mwanza zimeharibu miundombinu ya barabara ikiwemo madaraja wilayani Sengerema huku mtu mmoja dereva wa lori akisombwa na maji wakati akijaribu kuvuka mto Bugakala.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella Jumatatu Aprili 27, 2020 alifika katika maeneo yaliyoathirika ikiwemo Nyamazugo (Kamanga-Nyamazugo), Ibondo (Sengerema, Ibondo-Kasungamile) pamoja na Nyanchenche (Sengerema-Nyanchenche-Nyang'hwale) ili kubaini uharibifu uliotokea kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mawasiliano katika barabara ya Kamanga-Nyamazugo ilikata mawasiliano kufuatia mvua iliyonyesha Jumamosi Aprili 25, 2020 na hivyo kutatiza usafiri wa abiria na mizigo kutoka na kwenda Halmashauri ya Buchosa kupitia barabara hiyo.
 Eneo la mto Bugakala wilayani Sengerema likiwa limefurika maji kufuatia mvua iliyonyesha Jumamosi Aprili 25, 2020 na hivyo kutatiza mawasiliano baina ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza na Nyang'hwale mkoani Geita.
 Lori likiwa limekwama mto Bugakala wilayani Sengerema baada ya mto huo kufurika maji na daraja kukatika kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali kutembelea miundombinu ya barabara iliyotatizika kutokana na mvua wilayani Sengerema.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.