LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Misungwi apokea vifaa vya kupambana na Corona “ni wakati wa kufanya kazi”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Juma Sweda amewahimiza wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji mali huku wakichukua tahadhari dhidi ya Corona.

Amesema si vyema shughuli za kimaendeleo ikiwemo kilimo kusimama kutokana na janga la Corona kwa kuwa hatua hiyo inaweza kuleta madhara zaidi kwa wananchi.


DC Sweda ameyasema hayo Mei 18, 2020 wakati akipokea vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona vilivyotolewa na shirika la ASAP linalotekeleza mradi wa kuboresha elimu katika Kata ya Idetemya wilayani Misungwi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mratibu Miradi wa Shirika la ASAP (Africa School Assistance Project) Mkoa Mwanza, Jackson Nzemye akitoa taarifa ya vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Corona vilivyotolewa na shirika hilo wilayani Misungwi.
Mkuu wa Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Juma Sweda (kulia) akipokea vifaa vya kupimia joto la mwili (Thermometer) vilivyotolewa na shirika la ASAP.
Zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia mapambano dhisi ya Corona limefanyika katika Kata ya Idetemywa wilayani Misungwi.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akikagua maabara ya masomo ya Sayansi iliyojengwa na shirika la ASAP kwa kushirikiana na wananchi pamoja na Halmashauri ya Wilaya Misungwi katika Shule ya Sekondari Idetemya.
Mwonekano wa jengo la maabara ya masomo ya Sayansi katika Shule ya Sekondari Idetemya wilayani Misungwi.
Tazama BMG TV hapa chini
Tazama hapa chini mabweni ya kisasa yaliyozinduliwa na Makamu wa Rais-Misungwi

No comments:

Powered by Blogger.