LIVE STREAM ADS

Header Ads

PICHA: Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia mkoani Kigoma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limeratibu maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Wilaya Kasulu mkoani Kigoma na kutumia fursa hiyo kutoa elimu kwa jamii kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake na watoto. 

Maadhimisho hayo yamefanyika Jumatatu Disemba 07, 2020 katika uwanja wa Mashujaa Halmashauri ya Mji wa Kasulu yakitanguliwa na maandamano ya wanaharakati wa kupinga ukatili wa kijinsia kuanzia uwanja wa Shule ya Msingi Kiganamo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally amesema baadhi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyolalamikiwa wilayani Kasulu ni pamoja na wanaume kutelekeza familia na kusababisha ongezeko la watoto wanaoishi mitaani hivyo elimu inaendelea kutolewa ili kupambana na hali hiyo. 

Naye mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Kamanda wa Polisi wilayani Kasulu Idd Kiogomo amewaasa wanajamii kushikamana na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kuwafichua wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia ili hatua stahiki zichukuliwe. 

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia hufanyika kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 10 ambapo wadau mbalimbali hutumia fursa hiyo kutoa elimu kwa jamii kutojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally (wa pili kushoto) akiungana na wadau mbalimbali kwenye maandamano ya kupinga ukatili wa kijinsia wilayani Kasulu.
Kauli mbinu "Tupinge Ukatili wa Kijinsia, Mabadiliko Yanaanza na Mimi".
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa Shirika la UN WOmen nchini Tanzania, Juliana Brousard (kulia) ambao ni miongoni mwa wafadhili wa shughuli za shirika la KIVULINI ambalo kwa Mkoa Kigoma linatekeleza mradi wa kupinga ukatili wa kijinsa katika Wilaya za Kasulu, Kakonko na Kibondo.
Elimu ikitolewa kwa njia ya sanaa.
Mkuu wa Dawati la Jinsia la Polisi Wilaya Kasulu, Maimuna Abdul amesema kuanzia mwezi januari hadi Novemba mwaka huu jumla ya kesi 153 za ukatili kwa watoto zimeripotiwa ambapo kati ya hizo mimba za utotoni ni 42 na ndoa za utotoni ni saba na jitihada za kupambana na matukio hayo zinaendelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Kasulu Mji, Lucy Njovu.
Afisa wa shirika la KIVULINI.
Kamanda wa Polisi wilayani Kasulu Idd Kiogomo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.