LIVE STREAM ADS

Header Ads

SILINDE: Tutafuatilia kwa ukaribu zoezi hili, Rais amenituma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, David Silinde amesisitiza kuwa Serikali itafuatilia kwa ukaribu zoezi la kuwabaini watoto wenye mahitaji maalum ambao tayari wamefikisha umri wa kwenda shule wa kuanzia miaka minne hadi sita lililoanza Januari 09-21, 2021.

Silinde alitoa kauli hiyo jijini Mwanza wakati akifunga mafunzo elekezi kwa maafisa maendeleo, ustawi wa jamii, elimu maalumu pamoja na wauguzi watakaoshiriki kwenye utekelezaji wa zoezi hilo linalolenga kuwabaini watoto wenye ulemavu nchini ili kuboresha mahitaji yao kielimu.
Washiriki wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza Januari 04-06, 2021.
Washiriki hao walijengewa uwezo ili kutekeleza vyema zoezi hilo la kuwatambua watoto wenye mahitaji maalumu ili wapate elimu stahiki kulingana na hali yao.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.