LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la EMEDO lakutana na wadau kujadili Mwongozo wa Kuendeleza Uvuvi Mdogo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Shirika la EMEDO limewakutanisha wadau mbalimbali wa uvuvi jijini Mwanza ili kuwajengea uwezo wa kutambua na kutekeleza mwongozo wa hiari wa kuendeleza uvuvi mdogo kwa muktadha wa uhakika wa chakula na kuondoa umaskini.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Edtrudith Lukanga amesema baada ya wadau hao kujengewa uwezo ili kuutambua vyema mwongozo huo, wataweza kujadili kutoa maoni kupitia mtandao wa “Small-Scale Fisheries Resource & Collaboration Hub” na kueleza ikiwa mwongozo huo unatekelezeka ama unahitaji kuboreshwa zaidi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa shirika la EMEDO, Edtrudith Lukanga akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Afisa Uvuzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kenedy Kitinusa akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Wadau mbalimbali wakichangia mada wakati wa warsha hiyo.
Picha ya pamoja...
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.