LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wajasiriamali waishukuru taasisi ya DSIK Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wajasiriamali vijana jijini Mwanza waliopata mafunzo ya elimu ya fedha kutoka taasisi ya DSIK Tanzania wameishukuru taasisi hiyo wakisema elimu waliyoipata itawasaidia kukuza biashara zao.

Baadhi ya wajasiriamali waliopata mafunzo hayo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya akiba duniani 2022, wamesema yatawasaidia kukabiliana na changamoto zilizokuwa zinawakabili ikiwemo kukosa ujuzi rahisi wa kutunza kumbukumbu.

Mariam Yunis pamoja na Mwamvua Mikidadi walisema mafunzo hayo yamewajengea nidhamu ya fedha hususani kutambua umuhimu wa kuweka akiba kwa ajili ya manufaa ya baadae ikiwemo kukuza mitaji.

“Tunaomba Serikali iendelee kutoa mafunzo kwa vijana, kurahisisha upatikanaji wa mikopo isiyo na riba inayotolewa na Halmashauri ili tuondokane na changamoto ya kukopa kwenye taasisi zinzokopeshwa kwa riba kubwa kwani tunashindwa kurejesha na kusababisha biashara zetu kufa” walishauri Felista Bundala pamoja na Magdalena Leonard.

Naye Mkufunzi wa Elimu ya Fedha kutoka taasisi ya DSIK Tanzania, Emmanuel Walwa alisema taasisi hiyo imekuwa ikitoa mafunzo kwa wajasiriamali vijana hususani mabinti, wanawake wanachana wa SACCOS pamoja na wanafunzi katika shule za msingi na sekondari jijini Mwanza ili kuwajengea uwezo wa kusimamia biashara kwa ufanisi.

Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku mbili Oktoba 24-25, 2022 jijini Mwanza yakiwashirikisha vijana wajasiriamali 50 ambapo Wiki ya Akiba Duniani huadhimishwa wiki ya mwisho ya mwezi Oktoba kila mwaka ikilenga kuhimiza umuhimu wa jamii kuweka akiba kwa manufaa ya baadae.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkufunzi wa Elimu ya Fedha kutoka taasisi ya DSIK Tanzania, Rukia Amin akiwasilisha mada kwenye mafunzo kwa vijana wajasiriamali jijini Mwanza.
Wajasiriamali wakifuatilia mafunzo hayo.
Mkufunzi wa Elimu ya Fedha taasisi ya DSIK Tanzania, Rukia Amin akiwasilisha mada kwenye mafunzo 
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakijadili jambo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali.
Mkufunzi wa Elimu ya Fedha kutoka taasisi ya DSIK Tanzania, Emmanuel Walwa akielezea umuhimu wa mafunzo ya elimu ya fedha kwa wajasiriamali.
Mjasiriamali Mariam Yunus akielezea umuhimu wa mafunzo hayo.
Mjasiriamali Mwamvua Mikidadi akizungumzia mafunzo hayo na umuhimu wake.
Mjasiriamali Felista Bundala akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mjasiriamali jijini Mwanza, Magdalena Leonard akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.