LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri wa Utalii afungua Maonesho ya Utalii Karibu Kusini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wazii wa Maliasiali na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amefungua maonyesho ya pili ya kimataifa ya Karibu Kusini katita viwanja vya Kihesa Kilolo mkoani Iringa lengo likiwa ni kutangaza vivutio vya kitalii vilivyo Kanda ya Kusini.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza wakati wa kufungua maonyesho hayo, Waziri wa Balozi Dkt. Chana alisema imefika zamu ya kuvitanga vivutio vya kitalii vilivyo Kusini ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Kanda hiyo na pia kuongeza pato la taifa.

Balozi Dkt. Chana alisema Serikali itatumia maonyesho ya kimataifa ya Karibu Kusini kama sehemu ya mkakati kutekeleza Ilani ya CCM ya kufikisha watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025 na kwamba Wizara ya Maliasili imejipanga kimkakati ili kufikia malengo hayo ikiwezekana kuvuka idadi hiyo ya watalii.

Alisema maonyesho hayo yamefunguliwa rasmi yakihusisha mikoa kumi ya kusini mwa Tanzania ikiwa ni sehemu mwafaka yakutangaza utalii wa kusini.

Balozi Dkt. Chana alisema mikoa inayoshiriki maonyesho hayo ni mkoa wa Iringa, Morogoro, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Ruvuma, Lindi na Mtwara ambapo mikoa hiyo kwa kutumia maonyesho hayo itasaidia kutangaza vivutio vya utalii kusini mwa Tanzania.

Alisema maonyesho hayo ya karibu kusini yenye kaulimbiu inayosema “uwekezaji,kusinifahari yetu” ni jukwaa ambalo linawakutanisha wadau mbalimbali katika sekta ya utalii kwa lengo la kuuza bidhaa, kutafuta masoko pamoja na kujenga mahusiano ya kibiashara kwenye sekta mbalimbali za kitalii.

Balozi Dkt. Chana alisema kutokana na kampeni ya filamu ya Tanzania 'The Royal Tour' ilifanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan imesaidia kuongeza idadi ya watalii kutoka 922,692 mwaka 2019 hadi kufukia watalii 1,034,180 mwaka huu.

Alisema mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imebarikiwa vivutio vingi vya kitalii ambapo mradi wa REGROW unasaidia pia kuvitangaza vivuti hivyo na kujenga kituo cha utalii wa kusini mwa Tanzania katika eneo la Kihesa Kilolo ambacho kitatumia zaidi ya bilioni 12.

Balozi Dkt. Chana alisema Serikali ya awamu ya sita imeendelea kujenga viwanja vya ndege kwa lengo la kukuza na kuitangaza sekta ya utalii ili kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ya Tanzania.
Na Fredy Mgunda, Iringa

No comments:

Powered by Blogger.