LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Mkuu azindua Mpango Mkakati wa AMREF 2023-2030

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu kuhusu historia ya AMREF nchini kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Septemba 15, 2023.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu kuhusu historia ya AMREF nchini kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Septemba 15, 2023.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu kuhusu historia ya AMREF nchini kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Septemba 15, 2023.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (aliyevaa suti ya bluu) akikata utepe ishara ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030, Septemba 15, 2023.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (aliyevaa suti ya bluu) akikata utepe ishara ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030, Septemba 15, 2023.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF nchini, Dkt. Florence Temu kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Septemba 15, 2023.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030, Septemba 15, 2023. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya AMREF Tanzania Anthony Chamungwana, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Mazrui , Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa AMREF Health Africa Tanzania wa Mwaka 2023-2030 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Septemba 15, 2023. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya AMREF Tanzania Anthony Chamungwana, Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Florence Temu, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Mazrui , na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila.
Shirika la Amref Health Africa, Tanzania limezindua mpango mkakati wa kipindi cha mwaka 2023-2030.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, na unalenga kuunga mkono na kuboresha huduma bora za afya kwa Watanzania kupitia lengo lake la kuendeleza na kuboresha huduma muhimu za afya zitakazoongozwa na jamii na watu wa jamii hizo, huku ikizingatia kushughulikia Vibainishi vya afya vya kijamii (Social Determinants of Health).

Kwa miaka thelathini na sita (36) sasa, Shirika la Amref Health Africa Tanzania limekuwa likishirikiana na Serikali ya Tanzania hususani Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na wadau wengine katika kuboresha mifumo mbalimbali ya afya nchini. Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa aliipongeza Amref Health Africa Tanzania kwa kusaidia juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata huduma bora za afya.

"Nafurahi kwa kuwa Mpango mkakati huu mpya wa Amref Tanzania unajikita katika kuboresha Afya ya msingi yaani Primary Health care kwa kupitia programu zilizotajwa, huku ikiangazia vibainishi vya kijamii vya afya (Social determinants of health). Naelewa kukabiliana na changamoto hizi inahitajika jitihada za wadau wa kada mbalimbali kushirikiana ili kuleta tija” amesema Waziri Mkuu.


Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Amref Health Africa, Dkt. Githinji Gitahi amesema "Mwezi Machi 2023, Shirika la Amref Health Africa lilizindua mpango mkakati wa miaka minane nchini Rwanda na maeneo ya kipaumblele yanalandana vyema na yale tajwa katika mpango mkakati wa Amref Tanzania kwani kama nilivyosema changamoto za bara la Afrika zinafanana kwa kiwango kikubwa. Mpango mkakati huu umejikita kuleta majibu ya changamoto zinazotokana na viashiria vya mabadiliko yanayotokea barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla ikichochewa na sera za Bara la Afrika na Ulimwengu kwa ujumla ambazo zinaunda afya ya waafrika."

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa nchini Tanzania, Dkt. Florence Temu amesema kuwa mpango mkakati huo utatoa mwelekeo kwa Amref Tanzania katika kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuwekeza katika mifumo ya afya inayoongozwa na jamii na inayolenga watu kwa ajili ya huduma endelevu za afya ya msingi.

"Katika mpango mkakati wetu, ambao utadumu kwa miaka nane (2023-2030), tunajitahidi kuhakikisha kuwa jamii nyingi zinafikia na kunufaika na huduma za afya ya msingi. Lengo letu ni pamoja na kuwekeza katika huduma ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wote na kushughulikia masuala ya kijamii yanayochangia kuenea kwa magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) na magonjwa mengine, ikiwa ni pamoja na magonjwa yanayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa" amesema.

"Tunalenga kuimarisha uwezo wa jamii zetu na mifumo ya afya kwa kushughulikia athari za kiafya zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa kujifunza kutokana na mlipuko wa COVID-19, tunataka kuongeza uwezo wa sekta ya afya kukabiliana na milipuko. Aidha, tutawawezesha wanawake na vijana kupitia elimu na hatua za kuboresha ubora wa maisha kwa kutambua uhusiano muhimu kati ya ubora wa maisha na matokeo ya afya" ameongeza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Amref Health Africa Tanzania, Anthony Chamungwana amesisitiza dhamira ya Amref katika kusaidia juhudi za serikali katika kukuza huduma za afya nchini.

"Tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na serikali na wadau wengine ili kuhakikisha kuwa jamii zinapata huduma bora na nafuu za afya. Tutaendelea kuwekeza katika huduma rafiki kwa watumiaji kulingana na miongozo ya nchi, na kuhakikisha utekelezaji wa kiwango cha juu kutoka ngazi ya jamii hadi ngazi ya kitaifa" amesema.

Mpango mkakati huu wa 2023-2030 unatokana na uzoefu wa Amref Tanzania kutokana na utekelezaji wa mikakati ya awali pamoja na vipaumbele na mwelekeo wa sasa wa kimataifa na kitaifa. Kuongezeka kwa upatikanaji na matumizi ya huduma za afya, kusaidia rasilimali watu kwa afya, na kuhamasisha uwekezaji katika afya bado ni miongoni mwa maeneo ya kipaumbele kwa mkakati wa sasa.

Mkakati huu unaweka mkazo zaidi katika kuimarisha mifumo ya afya ya jamii kwa ajili ya kuboreshwa kwa upatikanaji, matumizi, na usimamizi wa huduma katika ngazi ya jamii. Pia unalenga kushughulikia viashiria vya kijamii vya afya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na utayari wa vitisho vinavyoeza jitokeza.

Amref Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wizara zote, mashirika ya serikali, wafadhili, mashirika ya kijamii (CBOs), mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), sekta binafsi, na wanajamii. Kupitia utekelezaji wa mkakati huu, Amref Health Africa Tanzania inatarajia kuchangia upatikanaji sawa na endelevu wa huduma bora za afya ya msingi (PHC) na hatimaye kuchangia katika kufanikisha huduma ya afya kwa wote (UHC) nchini Tanzania.

No comments:

Powered by Blogger.