Header Ads

Pamba washindwa kutamba mbele ya Kagera Sugar ugenini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Timu ya soka ya Kagera Sugar imekomaa na kusalia ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao wa 2019/20 baada ya kupata ushindi wa nyumbani kwenye mchezo wa marudioano dhidi ya Pamba SC uliopigwa jumamosi Juni 08, 2019 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoka.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza Jumatatu Juni 03, 2019, timu hizo zilitoka uwanjani kwa suluhu ya 0-0. Mechi hizo za mtoano (Play-Off) zilikuwa zikilenga kupata timu moja itakayopanda ligi kuu baada ya Kagera Sugar kumaliza nafasi ya 18 msimu uliomaliza wa 2018/19 huku Pamba SC ikimaliza nafasi ya pili katika kundi B kwenye ligi daraga la kwanza msimu wa mwaka 2018/19.
Tazama video hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.