LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKONGORO: Jumuiya za CCM ziwasaidie wenye uhitaji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa Mwanza, Nyirizu Makongoro ametoa rai kwa Jumuiya za Chama hicho kuwa na utamaduni wa kusaidia mahitaji ya kibinadamu kwa makundi mbalimbali yenye uhitaji katika jamii ikiwemo watoto yatima, wenye ulamavu pamoja na wazee.

Makongoro aliyasema hayo Mei 15, 2021 kwenye sherehe ya Eid pili (Eid El Fiitr) iliyoandaliwa na jumuiya ya wazazi (CCM) Kata ya Butimba wilayani Nyamagana iliyoambatana na utoaji msaada wa mahitaji mbalimbali kwa makundi ya watu wenye uhitaji katika Kata hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa Mwanza, Nyirizu Makongoro akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa Mwanza, Nyirizu Makongoro akiwakabidhi mahitaji mbalimbali ikiwemo sabuni, sukari, mchele na mafuta ya kula wazee wa Kata ya Butimba wilayani Nyamagana.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa Mwanza, Nyirizu Makongoro akiwakabidhi bidhaa mbalimbali wazee katika Kata ya Butimba, Nyamagana.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa Mwanza, Nyirizu Makongoro akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu msaada wa bidhaa mbalimbali.
Watoto wenye mahitaji maalumu wakipokea msaada ya bidhaa mbalimbali.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa Mwanza, Nyirizu Makongoro akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu msaada wa bidhaa mbalimbali.
Katika hafla hiyo, Makongoro pia alisaidia upatikanaji wa fedha zaidi ya shilingi laki sita, rangi ndoo 10 pamoja na mifuko 20 ya simenti kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Butimba ambayo tayari imepauliwa.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.